WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA
*Asisitiza kwamba kazi ndiyo msingi wa maendeleoWAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na maarifa
kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Pia
amewasihi wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani wahakikishe
suala la kulinda mipaka hiyo linapewa kipaumbele ili kuimarisha amani na
utulivu nchini.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo
leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wananchi
alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.Waziri
Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
amesema ili vijana waweze kupata maendeleo lazima wafanye kazi kwa
bidii.Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo
kuwakumbusha wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani washirikiane
na Serikali katika kuimarisha ulinzi na usalama.Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ukarabati wa kituo cha afya cha
Kata ya Mbekenyera na kuwaeleza wananchi dhamira ya Serikali ya
kuwahudumia.Amesema Serikali imetoa sh.
milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya kujifungulia, maabara, wodi
ya wanawake na wanaume na chumba cha upasuaji.“Serikali
imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya
afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi
yao.”Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi
hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia
ili waweze kupata maendeleo.Pia, Waziri Mkuu
amekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika kituo hicho. Gari hilo
limetolewa na Rais Dkt. John Magufuli ili kuimarisha huduma za afya
kituoni hapo.IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAMOSI, MACHI 24, 2018.