Mkurugenzi SBL afanya mazungumzo na maofisa Idara ya Uhamiaji
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, jana
alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa ni
sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa
wafanyakazi wa kampuni hiyo. “Tukiwa kama kampuni inayoheshimu sheria
na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla, tumekuwa
tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha haki na maslahi ya
wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie SBL
imeajiri wafanyakazi zaidi ya 700 katika viwanda vyake vilivyopo Moshi,
Mwanza na Dar es Salaam. Bia yake mama ya Serengeti Premium Lager
ilizalishwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia kimea kwa aslimia 100 na
imeweza kushinda zaidi ya tuzo kumi za dhahabu za kitaifa na kimataifa.Tangu
kuanzishwa kwake mwaka 2002, SBL imekuwa huku ikiongeza idadi ya
bidhaa inazozalisha. Baada ya kisisi iikubwa cha hisa kuchukuliwa na
Kampuni ya Bia ya AFRIKA Mashariki (EABL)/Diageo mwaka 2010 kumekuwepo
uwekezaji mkubwa amboa umefanikisha uzalishaji w3a bidhaa zenye ubora
wa kimataifa na kutengeza fursa kwa Watanzania.Moja
kati ya nguzo za Diageo ambayo ni kampuni mama YA sbl ni kujenga na
kuwawezesha wafanyakazi wake sehemu yoyote inapofanya kazi ikiwamo
Tanzania. Kutokana na hili idadi ya wataalamu wageni imepungua kwa kiasi
kikubwa kutoka zaidi ya 30 hadi sita kufikia mwezi Machi 2018 ikiwa ni
chini ya asilimia 1 ya nguvu kazi katika kampuni“Tunapenda
kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuimarisha mahusiano na
wafanyakazi wetu. Tutaendelea kukidhi mahitaji yao kwa kuwahakikishia
bidhaa bora ikiwa ni sehemu muhimu kwa biashara yetu,”anasema mkurugenzi
huyo.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni