Jeshi la polisi mkoa wa mbeya linawashikiria
vijana kumi na wawili akiwemo kijana mmoja ambaye alifahamika kwa jina la alain
achile(22) mkazi wa airpot ya zamani.
Hayo ameyasema kamanda wa wa polisi mkoa wa
mbeya Mohamed mpinga wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kuhusiana na doria zinazofanya na
jeshi hilo.
Mpinga Amesema vijana hao walifanya vurugu
baada ya kutokea kifo cha alain achile na kusababisha jeshi la polisi kutumia
mabomu ya machozi ili kuzuia ghasia hizo.
Aidha amesema mtuhumiwa huyu pamoja na wenzake baada
ya kukamatwa walifikishwa kituo kikuu cha polisi mbeya mjini na
kufunguriwa mashitaka ya uzembe na
ukorofi.
Mnamo 25.03.2018 majira ya 10.45 asubuhi
mtuhumiwa alain achile alidhaminiwa na ndugu zake na kwenda nyumbani kwao na na
majira ya saa 18.00 jioni walipewa taarifa ya kifo cha cha alain achile.
Ameongeza kwa kusema vijana hao walikwenda
kufanya vurugu nymbani kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa boaz kazimoto(74)kwa
kumtuhumu kuwa ndiye aliyewaita polisi kumkamata marehemu.
Halikadhalika walikwenda ofisi ya afisa
mtendaji wa kata ya iyela na kubomoa milango yote,kuharibu samani na baadhi ya
nyaraka na kwenda nyumbani kwa askali H.4325 PC YOHANAwa kikosi caha kutuliza
ghasia na kuvunja yamadirisha ya nyumba
yake na kutoa kauli ya kuchoma nymba hiyo na kuvunja kuvunja gari ya polisi
wilaya ya mbeya mjini yenye usajili PT1987 aina ya toyota.
Kamanda amewataja watuhumiwa nane waliohusika
na vurugu hizo kuwa ni ELIUD DAUD(22),BARIKI MASUDI(30),ISSA NELSON(26),ROBART
MWANGUPILI(24)WAKAZI WA IYELA NA FRANK KILEMI(33),KRIST NELSON(33)ESTOM
MBALO(24)FELIX MBILINYI(21)WAKAIZ WA AIRPOT YA ZAMANI na upelelezi utakapo
kamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
Hata Hivyo MPINGA Amekana Kuhusika Kwa Jeshi La
Polisi Kuhusiana Na Kifo cha Alaini Achile Badala Yake Amefungua Jalada La
Uchunguzi (PE) Kupitia Ofisi Ya
Mkuu Waupelelezi Wa Amkosa Ya
Jinai(RCO)