Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la AHADI MGAYA
mwenye umri kati ya 30-33 mkazi wa mtaa wa mwafute kata ya ilemi mkoani mbeya
ameaga dunia baada ya kujinyonga usiku wa kuamkia leo.
Akiongea barozi wa mtaa
wa mwafute JAPHETI MAHINYA amesema kuwa
yeye alipewa taarifa ya marehemu kutoweka nyumbani jana kupitia mke wake na
marehemu kusema kuwa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo hakijafahamika kwani
hakuwa na mgogoro wowote.
Hata hivyo MAHINYA
ametoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi na badala yake kama
kutakuwa na tatizo au mgogoro wowote ni heri kushaulisha watu wanaokuzunguka
kabla ya kuchukua hatua yoyote.
Nao majirani wa
marehemu FRANCIS TAMIMU pamoja na SOPHIA wameeleza kupokea kwa mshituko tukio
hilo na kutoa wito kwa wananchi wengine kutokuchukua hatua za kujinyonga kwa
hupelekea maumivu makali kwa familia na jamii inayomzunguka.
Kwa upande wake kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa mbeya MHAMED MPINGA amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kutoa wito kwa wananchi kutokatisha maisha yao kwa namna yoyote ile
kwani huacha majonzi na simanzi kwa wanafamilia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni