Wananchi wa mtaa wa mapambano kata ya iyela wametakiwa kuchangia ujenzi wa vyoo unaoendelea katika shule ya msingi mapambano ili kufanya mwendelezo wa sehemu alipoishia mdau aliyekuwa akijenga vyoo hivyo ndele mwaselela.
Hayo yameelezwa na afisa mtendaji wa mtaa wa mapambano katika
kata ya iyela kizito nenalo katika mkutano wa wazazi uliofanyika katika viwanja
vya shule ya msingi mapambano uliofanyika mapema hii leo.
Nenalo amesema wananchi hawanabudi kutambua kuwa afya ya
mtoto inawahusu wote na hivyo wanapaswa kutoa mchango huo wa shilingi elfu tatu
ili kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika.pia amewapongeza baadhi ya wananchi
ambao wameonesha mwitikio mzuri katika suala hilo.
Mwenyekiti wa mtaa wa mapambano mwinjilisiti mwampetele
amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitoa kwa vitendo na siyo maneno ikiwa ni
pamoja na kuhudhuria mikutano inayoitishwa kwa lengo la kujua maendeleo ya mtaa
wao.
Kwa upande wake joji mwangonele ambaye ni mwenyekiti wa
kamati ya shule ya msingi mapambano amesema kuwa wazazi hawanabudi kutilia
mkazo katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao ili kuhakikisha yanakuwa
mazuri.
Nao baadhi ya wazazi waliohudhuria mkutano huo Richard
salingo pamoja na anastazi mwampashe wameeleza kuwa suala hilo wamelipokea
vizuri na kuwataka wale ambao bado wanasitasita katika masula haya ya maendeleo
kutokufanya hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni