Jumamosi, 24 Machi 2018

UJENZI WA VYOO SHULE YA MSINGI MAPAMBANO MBEYA



Wananchi wa mtaa wa mapambano kata ya iyela wametakiwa kuchangia ujenzi wa vyoo unaoendelea katika shule ya msingi mapambano ili kufanya mwendelezo wa sehemu alipoishia mdau aliyekuwa akijenga vyoo hivyo ndele mwaselela.

Hayo yameelezwa na afisa mtendaji wa mtaa wa mapambano katika kata ya iyela kizito nenalo katika mkutano wa wazazi uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi mapambano uliofanyika mapema hii leo.
Nenalo amesema wananchi hawanabudi kutambua kuwa afya ya mtoto inawahusu wote na hivyo wanapaswa kutoa mchango huo wa shilingi elfu tatu ili kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika.pia amewapongeza baadhi ya wananchi ambao wameonesha mwitikio mzuri katika suala hilo.
Mwenyekiti wa mtaa wa mapambano mwinjilisiti mwampetele amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitoa kwa vitendo na siyo maneno ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano inayoitishwa kwa lengo la kujua maendeleo ya mtaa wao.
Kwa upande wake joji mwangonele ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi mapambano amesema kuwa wazazi hawanabudi kutilia mkazo katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao ili kuhakikisha yanakuwa mazuri.
Nao baadhi ya wazazi waliohudhuria mkutano huo Richard salingo pamoja na anastazi mwampashe wameeleza kuwa suala hilo wamelipokea vizuri na kuwataka wale ambao bado wanasitasita katika masula haya ya maendeleo kutokufanya hivyo.

nini umhimu wa mahali?

wanawake walio wengi wamekuwa wakiteseka sana katika ndoa zao na huwa wanajifikiria sababu nini lakini hawana majibu.
yafuatayo ni maswali ya nkujiuliza juu ya suala la mahali;
(a)Adamu alitoa mahali kwa nani?

(b)kama mahali ni zawadi kwa wazazi wa mtoto wa kike,je mtoto wa kiume hajalelewa na wazazi?

Jumanne, 21 Novemba 2017

JIELIMISHE UPATE KUELIMIKA

wanawake walio wengi wamekuwa wakiteseka sana katika ndoa zao na huwa wanajifikiria sababu nini lakini hawana majibu.
yafuatayo ni maswali ya nkujiuliza juu ya suala la mahali;
(a)Adamu alitoa mahali kwa nani?

(b)kama mahali ni zawadi kwa wazazi wa mtoto wa kike,je mtoto wa kiume hajalelewa na wazazi?

Jumamosi, 22 Julai 2017

             VIJANA NI JESHI LENYE NGUVU

       Vijana wengi wanashindwa kuwa wabunifu na kukimbilia vijiweni ati hakuna ajira. badala ya kupata kile wanachokitafuta huambulia ngeo, magonjwa na hata kifo,Hii hutkea baada ya kuona maisha yakizidi kuwa magumu kila kukicha na hivyo kuamua ndipo hujiunga na makundi ya (a)kuvuta  bangi (b)ujambazi (c) umalaya{kujiuza}  pasipo kujali athari zitakazowakumba baadae.

                 Wito wangu kwa vijana tujitambue kuwa sisi ni nguzo ya taifa hivyo tukiangamia kwa UKIMWI na vifo mbalimbali taifa litakuwa halina nguvukazi,hebu tujitahidi tufanye kazi tuache uvivu.

VIJANA TUNAWEZA