Jumanne, 27 Machi 2018

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEKANUSHA KUTOHUSIKA NA KIFO CHA ALAIN ACHILE (22) MKAZI WA AIRPORT YA ZAMANI



Jeshi la polisi mkoa wa mbeya linawashikiria vijana kumi na wawili akiwemo kijana mmoja ambaye alifahamika kwa jina la alain achile(22) mkazi wa airpot ya zamani.
Hayo ameyasema kamanda wa wa polisi mkoa wa mbeya Mohamed mpinga wakati akizungumza na waandishi wa habari  mapema leo kuhusiana na doria zinazofanya na jeshi hilo.

Mpinga Amesema vijana hao walifanya vurugu baada ya kutokea kifo cha alain achile na kusababisha jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi ili kuzuia ghasia hizo.
Aidha  amesema mtuhumiwa huyu pamoja na wenzake baada ya kukamatwa walifikishwa kituo kikuu cha polisi mbeya mjini na kufunguriwa  mashitaka ya uzembe na ukorofi.

Mnamo 25.03.2018 majira ya 10.45 asubuhi mtuhumiwa alain achile alidhaminiwa na ndugu zake na kwenda nyumbani kwao na na majira ya saa 18.00 jioni walipewa taarifa ya kifo cha cha alain achile.

Ameongeza kwa kusema vijana hao walikwenda kufanya vurugu nymbani kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa boaz kazimoto(74)kwa kumtuhumu kuwa ndiye aliyewaita polisi kumkamata marehemu.

Halikadhalika walikwenda ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya iyela na kubomoa milango yote,kuharibu samani na baadhi ya nyaraka na kwenda nyumbani kwa askali H.4325 PC YOHANAwa kikosi caha kutuliza ghasia na kuvunja yamadirisha ya  nyumba yake na kutoa kauli ya kuchoma nymba hiyo na kuvunja kuvunja gari ya polisi wilaya ya mbeya mjini yenye usajili PT1987 aina ya toyota.

Kamanda amewataja watuhumiwa nane waliohusika na vurugu hizo kuwa ni ELIUD DAUD(22),BARIKI MASUDI(30),ISSA NELSON(26),ROBART MWANGUPILI(24)WAKAZI WA IYELA NA FRANK KILEMI(33),KRIST NELSON(33)ESTOM MBALO(24)FELIX MBILINYI(21)WAKAIZ WA AIRPOT YA ZAMANI na upelelezi utakapo kamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
Hata Hivyo MPINGA Amekana Kuhusika Kwa Jeshi La Polisi Kuhusiana Na Kifo cha Alaini Achile Badala Yake Amefungua Jalada La Uchunguzi (PE) Kupitia Ofisi Ya  Mkuu  Waupelelezi Wa Amkosa Ya Jinai(RCO)

Jumamosi, 24 Machi 2018

WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA



WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA

*Asisitiza kwamba kazi ndiyo msingi wa maendeleoWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Pia amewasihi wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani wahakikishe suala la kulinda mipaka hiyo linapewa kipaumbele ili kuimarisha amani na utulivu nchini.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wananchi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ili vijana waweze kupata maendeleo lazima wafanye kazi kwa bidii.Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani washirikiane na Serikali katika kuimarisha ulinzi na usalama.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ukarabati wa kituo cha afya cha Kata ya Mbekenyera na kuwaeleza wananchi dhamira ya Serikali ya kuwahudumia.Amesema Serikali imetoa sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya kujifungulia, maabara, wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha upasuaji.“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.Pia, Waziri Mkuu amekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika kituo hicho. Gari hilo limetolewa na Rais Dkt. John Magufuli ili kuimarisha huduma za afya kituoni hapo.IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAMOSI, MACHI 24, 2018.

Mkurugenzi SBL afanya mazungumzo na maofisa Idara ya Uhamiaji

Mkurugenzi SBL afanya mazungumzo na maofisa Idara ya Uhamiaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, jana alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa ni sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo. “Tukiwa kama kampuni inayoheshimu sheria na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla, tumekuwa tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha haki na maslahi ya wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie SBL imeajiri wafanyakazi zaidi ya 700 katika viwanda vyake vilivyopo Moshi, Mwanza na Dar es Salaam. Bia yake mama ya Serengeti Premium Lager ilizalishwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia kimea kwa aslimia 100 na imeweza kushinda zaidi ya tuzo kumi za dhahabu za kitaifa na kimataifa.Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, SBL imekuwa huku ikiongeza idadi ya bidhaa inazozalisha. Baada ya kisisi iikubwa cha hisa kuchukuliwa na Kampuni ya Bia ya AFRIKA Mashariki (EABL)/Diageo mwaka 2010 kumekuwepo uwekezaji mkubwa amboa umefanikisha uzalishaji w3a bidhaa zenye ubora wa kimataifa na kutengeza fursa kwa Watanzania.Moja kati ya nguzo za Diageo ambayo ni kampuni mama YA sbl ni kujenga na kuwawezesha wafanyakazi wake sehemu yoyote inapofanya kazi ikiwamo Tanzania. Kutokana na hili idadi ya wataalamu wageni imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka zaidi ya 30 hadi sita kufikia mwezi Machi 2018 ikiwa ni chini ya asilimia 1 ya nguvu kazi katika kampuni“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuimarisha mahusiano na wafanyakazi wetu. Tutaendelea kukidhi mahitaji yao kwa kuwahakikishia bidhaa bora ikiwa ni sehemu muhimu kwa biashara yetu,”anasema mkurugenzi huyo.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie,


Nape Nnauye: Mungu Aliniokoa na Mdomo wa Bunduki ya Wanyama Wasiopenda Haki Tanzania

Nape Nnauye: Mungu Aliniokoa na Mdomo wa Bunduki ya Wanyama Wasiopenda Haki Tanzania

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amezungumzia tukio la kutishiwa bastola wakati akitaka kuzungumza na waandishi wa habari nje ya Hoteli ya Protea lililotokea baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Nape amekumbushia tukio hilo la Machi 23, 2017 na kuandika, “mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwenyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi.”Katika ujumbe huo Nape aliweka picha yake ya video akizungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli hiyo kueleza masuala mbalimbali, huku akiwataka vijana kudai haki zao bila woga.Mtu aliyemtishia bastola Nape alikuwa pamoja na wenzake wawili ambao kwa pamoja walikuwa wakimlazimisha arudi kwenye gari lake na kuondoka, lakini mbunge huyo aligoma na ndipo (mtu huyo) aliporudi nyuma na kuchomoa bastola kutoka kiunoni kisha kumtishia kabla ya kutulizwa na mwezake.Baada ya tukio hilo watu hao walitoweka eneo hilo muda mfupi baadaye.Kufuatia tukio hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema mtu aliyemtishia bastola Waziri huyo wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hakuwa askari wa Jeshi la Polisi.Soma: Mwigulu: Aliyemtishia Nape bastola si polisiMwigulu alieleza hayo baada ya kufungua mkutano wa kazi wa mwaka wa maofisa waandamizi wa polisi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi wa Jeshi la Polisi uliofanyika mjini Dodoma.Hata hivyo, Mwigulu alikataa kueleza kwa undani kuhusu mtu huyo kwa kubainisha anatoka taasisi gani wala jina lake.
Mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwemyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi! pic.twitter.com/M6PqupQQWK— Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) March 23, 2018

Mbowe afunguka kumhofia Mbunge Msigwa

Mbowe afunguka kumhofia Mbunge Msigwa


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefunguka na kuonyesha wasiwasi juu ya Jeshi la polisi kutaka kuwabambikizia kesi za mauaji au uhaini ili waweze kuwekwa mahabusu muda mrefu.

Mbowe amesema hayo leo Machi 22, 2018 ikiwa ni siku ambayo yeye pamoja na viongozi wengine wa chama hicho wanatakiwa kufika katika kituo cha polisi kusikiliza wito wa jeshi hilo na kusema kuwa wamepata taarifa zingine kuwa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa anataka kuhusishwa katika shauri hilo ambalo wao wanalo.

"Tuna taarifa pia ya kusudio la kumuunganisha Mhe. Peter Msigwa, Mb, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika shauri hili. Lakini pia katika wakati nenda rudi hii ikiendelea, tuna taarifa (asante teknolojia) kuwa zinapangwa njama mahususi za kutubambikia viongozi wa Chadema kesi za mauaji au Uhaini ili kuhalalisha azma ya Watawala kutuweka mahabusu kwa muda mrefu, wakidhani kwa kufanya hivyo watakuwa wamefanikisha kufifisha na hata kuua kabisa uwepo wa Upinzani katika Taifa" alisema Mbowe

Leo Machi 22,  2018, mimi  Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na viongozi wengine waandamizi wa CHADEMA akiwepo Mhe Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Mhe. John John Mnyika, Mb na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar; Mhe Halima J.Mdee, Mb, Mwenyekiti wa Bawacha, Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe.John W. Heche, Mb, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti (Mara, Simiyu na Shinyanga) na Mjumbe wa Kamati Kuu; Mhe. Esther N. Matiko, Mb, Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Mara na Mweka hazina wa Bawacha Taifa wanatakiwa kufika Makao Makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano.

FURSA 150 ZA BIASHARA TANZANIA

Fursa 150 za Biashara na Miradi Mbalimbali Nchini Tanzania

1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na           Makampuni mbalimbali.
5.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa       vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k
34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa           vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51. Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi
       ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL,          AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe,                 vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo

majonzi na simanzi



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la AHADI MGAYA mwenye umri kati ya 30-33 mkazi wa mtaa wa mwafute kata ya ilemi mkoani mbeya ameaga dunia baada ya kujinyonga usiku wa kuamkia leo.

Akiongea barozi wa mtaa wa mwafute JAPHETI MAHINYA  amesema kuwa yeye alipewa taarifa ya marehemu kutoweka nyumbani jana kupitia mke wake na marehemu kusema kuwa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo hakijafahamika kwani hakuwa na mgogoro wowote.
Hata hivyo MAHINYA ametoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi na badala yake kama kutakuwa na tatizo au mgogoro wowote ni heri kushaulisha watu wanaokuzunguka kabla ya kuchukua hatua yoyote.
Nao majirani wa marehemu FRANCIS TAMIMU pamoja na SOPHIA wameeleza kupokea kwa mshituko tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi wengine kutokuchukua hatua za kujinyonga kwa hupelekea maumivu makali kwa familia na jamii inayomzunguka.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa mbeya MHAMED MPINGA amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kutokatisha maisha yao kwa namna yoyote ile kwani huacha majonzi na simanzi kwa wanafamilia.